Rais JPM Asisitiza Kubomolewa kwa Jengo la Tanesco " Lazima Libomolewe Hata Nusu Yake"

Rais JPM Asisitiza Kubomolewa kwa Jengo la Tanesco " Lazima Libomolewe Hata Nusu Yake"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwasabu yeye ndiye rais kwasasa tofauti na zamani alipokuwa waziri.

Rais amesema hayo mapema leo wakati akihotubia wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila.
“Nikiwa Waziri Mheshimiwa Pinda alinipinga kuhusu kubomoa jengo la TANESCO lakini kwa sasa hawezi kwasababu Mimi ndiye Rais, nilikaa kimya kwasababu ya kuogopa kufukuzwa”, amesema Rais Magufuli.
Aidha rais ameongeza kuwa Jengo hilo lazima libomolewe hata kama nusu yake ndio ipo kwenye hifadhi ya barabara basi itolewe kama ni lote basi liondolewe pamoja na jengo la wizara ya maji hivyo hivyo kwasababu sheria ni msumeno.

Pia rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwasababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara.
“Mwaka 1997 wakati nikiwa naibu waziri wa Ujenzi nilikuja Kimara wakati wa kubomoa eneo la Kimara hadi Ubungo nilisema hata waliobaki wapo ndani ya hifadhi ya barabara hivyo wasiendelee na ujenzi”, amesema Rais Magufuli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad