Rais Magufuli Awapa Ujumbe Huu Nape Nnauye, Hussein Bashe

Rais Magufuli Awapa Ujumbe Huu Nape Nnauye, Hussein Bashe
Rais John Magufuli amewataka wabunge wawili wa CCM, Nape Nnauye na Hussein Bashe, ambao michango yao bungeni imekosoa uendeshaji uchumi, wampelekee majina ya wawekezaji wanaokwamishwa ili awape kazi.

Wabunge hao wa Mtama na Nzega Mjini waliikosoa Serikali wakati wa kujadili Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye alishutumiwa na wabunge hao kumpotosha Rais, alisema wakati akihitimisha mjadala huo kuwa alipigiwa simu na mkuu wa nchi na kuelezwa hayo.

“Naomba ninong’one na Bunge lako tukufu. Mheshimiwa Rais Magufuli aliposikia huu mjadala, alinipigia simu na aliniambia hivi,” alisema Waziri Mpango.

“Waziri, mwambie ndugu yako mheshimiwa Nape na mheshimiwa Bashe kuwa nawataka sana hao wawekezaji kwenye ujenzi wa Standard Gauge Railway.

“Wawalete hata kesho niko tayari kuwapa reli ya kutoka Kaliua –Mpanda au Isaka-Mwanza au reli ya Mtwara-Mchuchuma hadi Liganga waijenge.

“Hayo ni maneno ya mheshimiwa Rais. Natumaini waheshimiwa husika will raise up to this challenge from his excellence the president (wataifanyia kazi changamoto ya mheshimiwa Rais.”

Akijibu hoja za wabunge hao na wengine, Dk Mpango alisema si kwamba Serikali imeiweka pembeni sekta binafsi bali bado haijakaa vizuri na wakati mwingine inakuja na masharti yasiyotekelezeka.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya vijana changsmkeni kutuletea wawekezaji WA kweli

    ReplyDelete
  2. Hapa raisi hujawaelewa hawa vijana sawasawa.uwekezaji unahitaji udhiriki ws kamati na kuwahudidha vyama vyote. Inahitaji fikra kubwa je ni muhimu sana kwa sasa na kwa manufaa ya watanzania, au kuna kitu kingine zaifi Tanzsnia inabidi iwekeze kwsnza na ni muhimu zaifi kwa watanzania kwa sasa.
    Pili. Kutotegemea ununuzi wa kila kitu nje ukijua inskubidi uwrkeze kwrnye viwanda vya watanzania kwsnza watengeneza midumari, na vyuma ili vijana wapate ajira nchini.
    Tatu, kuwaajili watanzsnia wafanyakaxi bali wataalamu toka nje.
    Nne. Wsnaonegotiste, hawajui namna ya kukaza ksmba ili kuona fsifa inabaki nchini.uxoefu wa haya mambo mengi mnayoyafanya hamna. Inabidi badala ya kumwingiza kila mtu atakayeuwekezaji nchini kwa manufaa yso, je ulikuwa mpango wetu wa maendeleo kwanza au wao
    Hii inaighalimu tsifa kwa kufanya mambo bila mpangilio bora na kamili.Bado hsmjatambua tufanye nini kwanza kwa maendeleo ya kweli yanayohitajika ili watu waendelee na waweze kujitegemea.
    Mwisho, umewaita hawa wa ccm na kila mpinzani hukumps chsnsi sawa. Waliwrkwa ndani mara nyingi sana. Wslipelekwa polisi mars nyingi sana. Hawa wa cm unawstret vingine je hii ni haki na usawa.inabidi kiongozi awe msawa kikazi mbona hapa sioni uamuzi sawa kama mlivyowasweka ndani mara nyingi watetezi hasa Chadema. Kuna nini.Ccm tu ndo haina mskosa kukodoa. Huu upendeleo wa kichama tumeanza kuuona zamani sana. Sasa uko wazi. Ni watoto wa ccm. Wanaruhusiwa kuchangia na kusikilizwa. Si wengine

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad