Rais Magufuli Kuhudhuria Kuapishwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais Magufuli Kuhudhuria Kuapishwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.

Taarifa ya serikali iliyotolewa leo na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi imethibitisha hilo.
Mhe. Kenyatta ataapishwa siku ya Jumanne, Novemba 28, 2017, jijini Nairobi, ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad