Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia

Rais Magufuli: Mizengo Pinda Ndiye Aliyenizuia Kubomoa Jengo la Tanesco Sasa Mimi Ndiye Rais Hakuna wa Kunizuia
Rais John Magufuli amesema hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa waziri wa ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza mbele ya waziri mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mizengo Pinda aliyehudhuria uzinduzi huo, Magufuli amesema wakati huo aliogopa baada ya kuzuiwa na waziri mkuu huyo, lakini sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia.

Akizungumzia ubomoaji unaoendelea sasa amesema, “Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi ndiye Rais. Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa.”

“Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji. Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye hifadhi ya barabara,” amesema.

Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato, mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dk Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo la Tanesco hadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.

Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dk Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.

Pinda wakati huo akiwa waziri mkuu alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na Baraza la Mawaziri.

Pinda, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia 2008 baada ya kujiuzulu kwa Edward Lowassa alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya.

Alisema Serikali inamuamini Magufuli kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.

Dk Magufuli akiwasilisha bajeti bungeni mwaka 2012/13, alizungumzia ubomoaji akisema siasa iachwe akisisitiza sheria zimepitishwa ikiwamo Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na ya hifadhi ya barabara iliyoanza tangu mwaka 1932.

Alizungumzia jengo la Tanesco alisema liko kwenye hifadhi ya barabara na kwamba hata kama asipolibomoa yeye kuna siku litabomolewa vinginevyo sheria ibadilishwe.

Novemba 15 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Magufuli alimuagiza wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuweka alama ya X katika jengo la Tanesco na Wizara ya Maji, sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.
Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna namna ya kuzungumza na kuwazungumzia watu wengine. Lakini kumtaja waziri namna hii mbele ya ukumbi wa watu na yeye yupo hii inanitia uchungu sana hata kama ni raisi. Kuna namna ya kuzungumza bila kumwaibisha mtu. Na kauli ya kusema mimi ni raisi ambayo naisikia kila wakati si nadhifu kwa kiongozi yeyote yule. Imekuwa ni mimi, mimi, mimi.Je ni mtu mmoja tu ambaye ni jembe ajidifie kila wakati na kuwadharalidha au kuwafunika watanzania nchi nnzima? Hawa wanaohama toka upinzsni hivi hawajaliona hili. Ni mtu mmoja kuchukua sifa ya kila kitu na kumfunika kila mtu hadharani namna hii.Ndugu Mizengo alikuwa sahihi alipotaka jambo hilo lijadiliwe na bunge. Unaona wazi alihusisha wizara na chombo kwa kufuata sheria na kuheshimu watu waliopewa madaraka ambao inabidi wahusishwe. Hizi ndizo heshima na utaratibu kioungozi. Nashangaa watu wengi viongozi kuunga mkono. Hii inaidhinisha wazi nguvu inatumika na amri moja bila kujali viongozi wengine husika ingawa amewateua lakini hawana madaraka yoyote . Wamefunikwa na kupokea amri toka juu. Na wengi wamekuwa pia waoga kama yeye alivyokuwa mwoga kufukuzwa kazi wakati ule. Hii sasa kaiweka wazi mwenyewe. Na wakuu wa mikoa wengi wamemwiga kuforce msmbo si kwa vile wanaamini bali ni waoga . Wakiogopa kutumbuliwa pia. Nchi ikijaa na viongozi waoga, kumwogopa mtu mmoja kwa kutetea maslahi ya kazi zao ujue haya si maendeleo ya kweli, ujue hawana uhuru wa kufanya wanaloliamini kwa manufaa ya uma, bali wanalazimishwa kumtii na kumridhisha raisi tu ili watunze kazi zao na kutetea matumbo yao.alisema atasimama hatavunja, na Makonda akasimamisha, kumbe ni geresha tupu. Taifa zima kuunga mkono, ni halali kusema haya yote yanayofanyika leo mengi ni kinyume cha sheria. Na hata mikataba ya madini, bado hatujapata kikubwa ambacho watanzania tunastahili hata.Na kwa vile sheria zetu dhaifu, na watu asilimia 90 ni waoga bado hatupo huru kifikra. Lakini ameweza kuwanyamazisha na kuwashauri wengi kijanja kwani wanahitaji kula. Kuanzia Dr Slaa, mkuu wa bacva, kafulila, masha, na dada sofia Simba. Hawa walisimama mbele kupinga uendedhaji kama kuu lakini njaa na woga wamedhafungwa midomo. Hii ni hatari kwa mwelekeo wa nchi hii.watu kushindwa kudimamia ukwei, uhuru, na mali za nchi hii na kukubali kwa punje tu ni hasara kwa taifa zima hasa kwa vijana na watoto ambao tungewasaidia kuwapa uhakika wa maisha yao, na kuwafunza uzalenfo wakiwa wadogo. Sasa ndugu yangu Masha aliyezungumzia uzalendo Marekani anaopewa mtoto kwa namna hii utampaje mtoto majivuno ya kujivunia chake bila woga, bila uhuru, bila ushujaa. Inanisikitidha sana kuona wasomi wanaohangaika bila kuwa na mhimiri wao mzito.kamwe nchi hataendelezwa na fikra za mtu mmoja. Ni aibu sana, lakini inashangaza hata nilofikiri ni majemedari wamenaswa pabaya. Ni wasio na elimu za juu, wakulima, wafugaji wanaoteseka, wanaudhurumiwa, kunyanyaswa na wapiga kura waliobomolewa, nyanganya ardhi ndio watumie kurabzao kuiondoa CCM madarakani. Na wasio na ajira. Di wanaopewa vibarua na wazungu. Ni nyinyi vijana mnaotaka kujitengenezea ajira zenu, lakini serikali haitaki kuwajengea mazingira mazuri. Ni hawa wasomi wanaotegemea waajiliwe na mkuu wanapotodha nchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad