Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta Kuapishwa Leo

 Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta Kuapishwa Leo
Leo Novemba 28, Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta anaapishwa ili kuweza kuiongoza nchi hiyo kwa mujibu wa sheria za Kenya, baada ya ushindi alioupata kufuatia uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017.

Uhuru Kenyatta ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo David Maraga ambayendiye yule aliyetengua matokeo ya ushindi wake baada ya uchaguzi wa Agosti 8 kwa amri ya mahakama, huku akiwa ameshikilia biblia ambayo ilitumiwa na marehemu baba yake Mzee Jomo Kenyatta alipoapishwa kwa mara ya kwanza kuiongoza nchi hiyo 1964 baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni, Desemba 12, 1963, na meza ambayo itatumika kukaa wakati wa kutia saini, ni ile iliyotumika na rais wa tatu wa nchi hiyo Mwai Kibaki wakati wa kuapishwa kwake.
Kutokana na Uhuru Kenyatta tayari alikuwa madarakani kama Rais kwa wamu yake ya kwanza, hatakabidhiwa jamvia ambao ni kama alama ya kuwa na kamanda mkuu wa nchi na Majeshi yote ya nchi hiyo.
Pia sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa na mataifa mengine ya Afrika, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. JOhn Pombe Magufuli, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Rwanda Paul Kagame na wengineo.
Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Taifa wa Moi Kasarani na zinataraijwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu, huku upande wa upinzani wakiwa wamegomea kuhudhuria sherehe hizo, wakidai hawamtambui Uhuru Kenyatta kama rais wa nchi hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad