Rais Mugabe Amtunuku Shahada Mke wa Jenerali Aliyemzuia

Rais Mugabe Amtunuku Shahada Mke wa Jenerali Aliyemzuia
Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano.
Marry Chiwenga alipata shahada ya MBA kulingana na shirika la habari la Zimbabwe.
Awali Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.
Alihudhuria sherehe za kuhitimu kwa mahafala kwenye mji mkuu Harare.
Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.
Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mugabe ni raisi mmoja mkongwe Afrika, Msomi wa hali ya juu, Wise man, Hekima na Patriotic, wengi Waafrica Maraisi hawafui dafu. Kumdharalisha namna hii na magenge hata elimu haziendani na vyeo vyao, wakitumika na majitu ya nje wanaoinyemelea Zimbabwe na Mali asili ya Zimbabwe. Mtakuja tambua muda si mwingi. Empty heded Africans who just want powers, Lini Waafrika watasoma yaliyopita yasirudie tena. Africa tunajitumbukiza wenyewe kwa mabepari.
    Aibu kubwa kwa bara letu. Tunapopata nafasi kusonga mbele, bado mabepari na mabeberu, wanajichomoza kupitia Wajinga.

    ReplyDelete
  2. Usomi wake unemsaidia nini kama ameshindwa kuelewa kikomo cha uwezo wake kuongoza na kutaka kuigeuza Zimbabwekuwa a monarch country kwa kutengeneza mazingira ya kuhand over power kwa mkewe. Je,ndio unavyotafsiri usomi wake?
    Kuna maraisi wengi ambao wako averaged educated lakini wamefanya vyema .hivyo usomi wake sio justification ya kukalia kiti kwa 37 years !!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad