Rais wa Cuba Raul Castro amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea kazkazini , Ri Yong Ho katika jitihada za kimataifa kujaribu kupunguza uhasama baina ya Korea kazkazini na Marekani unaochochewa na azma ya Korea Kaskazini kuunda silaha za kinyuklia
Japo Cuba yenyewe pia ina mvutano na utawala wa rais Trump, katika taarifa yao ya pamoja na serikali ya Pyongyang Bw. Raul Castro ametoa wito kuwe na suluhu ya amani kwa sintofahamu hiyo baina ya Marekani na Korea Kazkazini.
Licha ya vikwazo vya Marekani Cuba imedumisha uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kaskazini tangu miaka ya 60.