RC Makonda Awatangazia Vita Wanaume Wanaokimbia Majukumu Yao ya Kulea Watoto

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA Leo ametangaza kiama kwa Wanaume wenye michezo ya kuwazalisha Wanawake kisha kuingia mitini kwa kukwepa majukumu ya kulea mtoto jambo linalosababisha ongezeko la Watoto wa Mitaani na ombaomba.

Mheshimiwa MAKONDA amesema anataka kuongezea nguvu Idara ya Ustawi wa Jamii kwa kuuunda kamati ya Wanasheria Wabobezi kwaajili ya kuwapeleka Mahakamani Wanaume wanaotelekeza Familia na kuwaachia Wanawake mzigo wa Malezi.

Aidha amesema kuwa Kamati hiyo pia itafanya Marekebisho ya Sheria ya pesa ya matunzo ya mwezi Kwa Mtoto kisha kuwasilishwa Bungeni kwakuwa pesa inayotolewa ni ndogo na haiendani na maisha ya sasa.

Amesema ni lazima ifike Mahala Mwanaume anaposababisha Ujauzito kwa Binti atambue analojukumu la kuhudumia.

RC MAKONDA amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Vifaa vya Ultrasound 10 za kisasa Aina ya “GE Vscan Access” zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 150 kwa Hospital 10 zilizofanya vizuri katika kutoa huduma bora za Afya na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Amezipongeza Hospital, Zahanati na Vituo vya Afya vilivyofanikisha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa kinara wa huduma bora za Afya na Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto na kuwaasa Watoa huduma kuwa na lugha nzuri kwa Wagonjwa.

Kwa Upande wake Mshauri Mtaalamu wa Magonjwa ya Mama na Mtoto kutoka CRDB Dr BRENDA DIMELLO amesema Dar es Salaam imekuwa Mkoa wa kwanza kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kutokana na usimamizi thabiti wa RC MAKONDA na watendaji wa Afya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad