Saada Mkuya Amshukia Waziri wa fedha

Waziri wa Fedha wa utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Saada Mkuya amemshukia Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango kwa kuandaa mpango wa taifa wa maendeleo pasina kuihusisha Zanzibar.

Mkuya ambaye ni mbunge wa Welezo visiwani Zanzibar amesema Dk Mpango amekuwa na kawaida ya kutokujibu hoja ambazo zinatolewa na wabunge wa kutoka Zanzibar jambo ambalo limemsikitisha.

Akichangia leo Novemba 10 bungeni mjini Dodoma Mpango wa Maendeleo ya Taifa, Mkuya ambaye katika mchango wake alisikitishwa na jinsi Waziri Mpango anavyoitenga Zanzibar licha ya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nadhani taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili sasa Mheshimiwa Mwenyekiti  (Azzan  Zungu) cha kusikitisha na fedheha kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu likaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Mkuya

“Hili niliseme wazi mheshimiwa mwenyekiti kupitia kwako, mheshimiwa Waziri wa Fedha (Dk Mpango) wakati tunajadili bajeti Juni mwaka huu baadhi ya wenzangu tunaotoka upande wa pili wa Muungano tulichangia maeneo fulani fulani,” ameongeza

Mkuya akichangia kwa sauti ya msisitizo amesema ‘’Lakini kwa masikitiko makubwa mheshimiwa mwenyekiti hakuna eneo hata moja lililoguswa likajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia na mimi nilichukua hatua kwenda kumuuliza mheshimiwa waziri wa fedha mbona angalau hata hoja mbili ili nao waone ni sehemu ya muungano.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukiwavjuu ndani ya ccmbhuna shida. Ukitelemka tatizo. Hivi ndivyo ccm ifanyavyo kazi.wengi mnayaona mapungufu lakini bado mnasapoti chama sababu ni waoga wa kukosa ushujaa.wengi wenu ni mizigo sababu ingawa mnaujua udhaifu wa chama hiki bafo mbakiunga mkono. Basi accgeni kulalamika. Si mnayakubali wenyewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad