Naibu Katibu wa CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya amedai hayuko tayari kuondoka Chama cha Wananchi CUF na kwenda katika vyama vingine hata kama chama chake kina mgogoro na iwapo na ikitokea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikiamua kukifuta
chama hicho yeye atastafu siasa
Akifanya mahojiano maalumu na Nipashe, Sakaya amesema kwamba Mgogoro unaoendelea ndani ya chama chao ni wa Kikatiba na unafahamika kwa msajili wa vyama na kuongeza kama ikitokea kwamba CUF inafutwa basi yeye atastaafu siasa na siyo kuhama chama.
"Kwanza naamini CUF haiwezi kufutwa. Yaani hilo halipo pamoja na changamoto ya mgogoro iliyopo. CUF ina misingi yake na mgogoro uliopo ndani yake ni wa kikatiba. Kwa hiyo, mimi nikiamua kwamba sasa sitaki kuendelea kuwapo CUF, ninaacha siasa. Ninaendelea na mambo yangu mengine, eeeh" Sakaya
Sakaya ameongeza kwamba "Kwanza mimi sijawahi kuwa na kadi ya CUF pekee. Nakumbuka wakati tunaripoti Shule yaSekondari ya Wasichana Kibosho (mwaka 1986) tuligawiwa kadi za kijani (CCM) wakati ule nchini kulikuwa na chama kimoja. Baadaye nikiwa na akili yangu timamu kadi niliyoichukua ni ya CUF ambayo niliichukua mwaka 1995 na ninayo mpaka leo na nitaendelea kuwa nayo. .