Serikali imesema inampango mkakati mzuri katika kuendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi na kutoa ajira za uhakika kwa Watanzania ambao wanafanya shughuli hiyo.
Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amesma hayo akiwa Soko la Samaki Msasani wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi kwa wavuvi waliofanya vizuri katika mashindano yakuvua samaki kwa vitumbwi na ngalawa yalioandaliwa na taasisi ya Tuna ambapo mshindi wa kwanza alipata tsh 400,000, wapili tsh 300,000 na wa tatu tsh 200,000.
Alisema serikali imesema inampango na mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi ili sekta hiyo iweze kufanya vizuri na kusonga mbele zaidi
Meya alisema wavuvi wanapaswa kuwa wabunifu ili kusaidia sekta hiyo kufanya vizuri zaidi
Afisa Uvuvi wa Manispaa Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza katika kilele hicho amesema kama kuwa watahakikisha wavuvi wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili waweze kuinuka kwa kipato zaidi.