Serikali Yamuonya Mbunge Zitto Kabwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameionya Manispaa ya Kigoma- Ujiji pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuacha mara moja mawasiliano na ushirika wa ‘Open Government partinership (OGP)’ na kama ikiendelea kufanya hivyo basi itachukuliwa hatua kali.

“Nataka niionye Manispaa ya Kigoma waache mara moja, watekeleze maamuzi ya serikali, na wakiendelea kufanya mawasiliano kama wanavyofanya sasa serikali itachukua hatua kali zaidi,” amesema Waziri Mkuchika.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na Mbunge Zitto Kabwe na mojawapo likiwa ni Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na ushiriki wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na miji mingine inayotaka kuingia katika OGP.

“Andiko la OGP linasema kuwa nchi ikijitoa, basi na wanachama wake wote walioko ndani ya ile nchi shughuli zao zinakoma,” alisema Mkuchika.

Aidha Waziri Mkuchika alieleza kuwa kujitoa kwa Tanzania katika OGP, hakukufanywa kwa kumuiga mtu bali kwa kupima vigezo ambavyo iliviona vinafaa kwani ni taifa huru linalojitawala na kufanya maamuzi yake lenyewe pasipo kushurutishwa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkuchika..Huyu Dogo kasha anza kugonga misitimu. Netwaki anaipoteza.
    Unamchunia akizidisha unamridisha Mirembe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad