Serikali Yasema Haiwezi Kuajiri vijana Wote nchini

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde amesema kuwa si kweli kwamba serikali inaweza kuwaajiri vijana wote kwenye sekta ya umma ila inachokifanya ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara.

Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Joseph Kenani lililohoji,

Serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa je?, Ni lini sasa serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchini ambao kwasasa ni wengi wamerundikana mtaani.

“Katika adhma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hilo la vijana serikali,imekuja na mipango mikakakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri wote kwenye sekta ya umma, ndio maana kupitia programme nilizozisema serikali imeona ni vyema kuishirikisha sekta binafsi, lakini nakuona falsafa ya uchumi wetu wa viwanda lakini vilevile kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo ufugaji na biashara, ili kwa pamoja tuwe tumetengeneza nafasi nyingi kwa vijana ili tuwafanye vijana wengi wa Kitanzania kuamini kwamba nafasi za kazi ni lazima ziwe za maofisini,” amesema Mavunde.

“Kwa mujibu wa sera ya ajira, sera ya ajira imezungumza vyema kabisa tafsiri ya neno ajira maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato, kwahiyo serikali tunachokifanya ni kutengeneza nafais nyingine zaidi za ajira ili vijana wengi zaidi wapate nafasi za kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine.”

Bongo5
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad