Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na wenye ulemavu imesema kuwa tozo iliyowekwa katika daraja la kigamboni imefuata utaratibu wa kisheria, kanuni na hivyo itaendelea kuwepo .
Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo Jenista Muhagama, baada ya mbunge Zainabu Ndolwa kuhoji,
Je ni lini serikali itasitisha tozo za daraja la Kigamboni ili liweze kutumika kama madaraja mengine Ruvu na Wami?
“Daraja la kigamboni limejengwa na mfuko wa jamii wa NSSF ni kivuko ambacho kinachofanya kazi kama vivuko vingine tulivyo navyo nchini na vivuko vingine pia vimeweka mfumo wa utozaji wa Tozo kidogo ili kuhakikisha kwamba vivuko vile vinaendela kulindwa na kukarabatiwa ili kuendelea kufanya kazi kwahiyo nisema kwamba Tozo iliyowekwa katika Daraja la Kigamboni imefuata utaratibu wa Kisheria na Kikanuni na hivyo itaendelea kuwepo,” amesema Jenista.