Shule ya Kanali Kipingu "Lord Baden Powell Memorial" Yapigwa Mnada Kama Nyumba za Lugumi

Hekaheka zinaendelea kutikisa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar kwa kufanyika minada ya Nyumba za Lugumi, nako mkoani Pwani, Shule ya Sekondari ya Lord Baden Powell Memorial iliyopo Mpakani mwa Dar na Pwani inayomilikiwa na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu imeuzwa kwa ‘pesa mbuzi’ ya shilingi milioni 100.

Mnada huo umefanywa leo Jumamosi ya Novemba 25, 2017, majira ya saa 3:00 asubuhi na Kampuni ya Makama Investiment Ltd na kupatikana mteja aliyefikia dau hilo la shilingi milioni 100.

Hata hivyo, wawakilishi wa Makama Investment iliyoendesha mnada huo hawakuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari juu ya vigezo na taratibu walizozitumia kuendesha mnada huo kwani waandishi wetu walijaribu kuuliza ili kupata ufafanuzi na hata jina la mshindi, lakini wahusika walidai kuwa wana haraka ya kwenda kwenye mnada mwingine ambao wangeliufanya huko Kigamboni, Dar.

Mtandao huu umezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Kanali Staafu, Idd Kipingu na kueleza kutoridhishwa na namna mnada huo ulivyoendeshwa kwani ulifanyika wakati kuna zuio la mahakama la kuuzwa kwa shule hiyo ambayo inadaiwa na benki shilingi milioni 38 na milioni nne ambazo ni za waendeshaji wa mnada.

Alisema kuwa, haiingii akilini shule yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 kuuzwa kwa milioni 100 lakini halaumu walioendesha zoezi hilo kwani nao watakuwa wamepewa maelekezo maalum.

“Tumekuwa na mazungumzo mazuri tu na wanaonidai ambao ni benki na tayari nimewaambia kwa kipindi cha miezi hii hali yangu siyo nzuri, lakini niliwaambia kuanzia miezi ijayo ningelianza kuwapia,” alisema Kanali Kipingu.
Kwa taarifa kamili, tembelea Global TV Online.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad