Simba hao walionaswa na mpiga picha maarufu duniani, Paul Goldstein zimeleta gumzo nchini Kenya wengi wakishangaa kitendo hicho wakiamini kuwa haijawahi kutokea kwa wanyama.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa Bodi ya Uanishaji wa Filamu nchini humo, Dr Ezekiel Mutua amesema ameziona picha hizo na ni kweli tukio hilo limetokea kwenye Mbuga ya Masai Mara huku akikiri kuwa endapo tukio hilo limefanyika kwa Simba hao basi dunia itakuwa hatarini kupoteza baadhi ya viumbe kwa siku za usoni.
Dkt. Mutua amesema kuwa ataagiza wanasayansi kuwachunguza Simba hao na kuwatenga kwenye mbuga hiyo ili kuepusha vitendo kama hivyo kwa Simba wengine.
“Hawa wanyama wanatakiwa wafanyiwe ushauri, huenda walishawahi kuwaona watu wakifanya mchezo huo mchafu hususani watalii mbugani hapo. Wanastahili kutengwa kwenye mbuga hiyo wabaki wenyewe.“amesema Dkt. Mutunga kwenye mahojiano yake na mtandao wa Nairobi News.
Hata hivyo Dkt. Mutunga amesema Bodi yake haihusiani kabisa na masuala ya wanyama lakini kwa tukio hilo hawezi kukaa kimya kulizungumzia.
“Bodi ya (KFCB) hatusimamii wanyama lakini hatuwezi kuacha kuongelea tukio hilo kwani haijawahi kutokea nchini Kenya kuona simba wawili wanaume wakifanya mapenzi. Kunauhitaji wa tafiti za kina kufanyika ili kuweza kubaini kama Simba hao ni kweli walikuwa wanaume wote.“amesema Dkt. Mutua.
Dkt. Mutunga amedai kuwa vitendo hivyo huwa vinaenea kwa njia ya filamu au Tv, ila anashangaa kwa wanyama kama hao wamewezaji kufikia maamuzi ya kufanya mapenzi ya jinsia moja huku akiamini kuwa kuna nguvu ya shetani imefanya kazi kwa wanyama hao.
“Wapi ulishawahi kuona wanyama wa jinsia moja wakishiriki mapenzi? Nadhani ni nguvu ya kishetani imeingia kwa simba hao.“amesema Dkt. Mutunga.
Mpiga picha wa tukio hilo, Goldstein amesema wakati yupo Masai Mara aliona simba wawili wakilaliana mwanzoni alijua ni jike lakini alipokaribia akakuta yote ni madume na kudai kuwa alishikwa na butwaa kwa kile alichokiona.
“Lilikuwa ni tukio la kustaajabisha machoni mwangu niliwahi kusikia tu kuwa lilishawahi kutokea Botswana lakini kwa niliyoyaona ni mageni mashoni mwangu.“amesema Goldstein.
TUKIO HILO LA WANYAMA WA JINSIA MOJA KUINGILIANA KIMWILI LINAELEZWAJE?
Wanasayansi na Wataalamu wa masuala ya wanyama na wadudu wanasema kuwa kuna baadhi ya wanyama huingilia kimwili bila kujali jinsia.
Mwanazoloji, Petter Bockman akirejea kwenye nadharia za Darwin amesema kuwa wapo wanyama na ndege zaidi ya aina 450 hufanya mapenzi ya jinsia moja ila kwa vile binadamu huwa hatufuatilii ni ngumu sana kuwakuta kwenye hali kama hiyo.
Akitoa mfano wa wanyama na ndege hao amesema kuwa ni Paka, Simba, kuku, kware, Nyangumi na wengine wengi.
Cheki baadhi ya maoni ya wadau mitandaoni baada ya kusambaa kwa picha hizo nchini Kenya.
Bongo5