Siri ya Wema Sepetu Kupukutika Mwili Yafichuka

VYUMA vimekaza? Siri ya staa mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kupukutika imefichuka baada ya picha zake kusambaa zikimuonesha akiwa hana lile shepu aliloliimba Dogo Aslay.

Kufuatia ishu hiyo, mashabiki wa Wema walipigwa na butwaa jinsi mwili wake huo ulivyopukutika. Ili kumaliza ubishi huo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Wema na kumuuliza kulikoni kupukutika mwili ambapo alisema kuwa, huko nyuma alikuwa hapendi kabisa kujihusisha na mambo ya kwenye ‘gym’ kwani alikuwa akiona hawezi kufanya hivyo kwa ajili ya kupunguza mwili, lakini siku zinavyozidi kusonga aliona ni bora kufanya hivyo kwa sababu mwili wake uliongezeka kupita kiasi.

“Unajua nilikuwa nikiangalia kila nguo ninayovaa inanibana. Wakati mwingine ni kubwa kabisa, lakini inakuwa hainitoshi, nikaona nina kila sababu ya kupunguza huu mwili ambao siyo mzuri hata kiafya,” alisema Wema.


Wema ambaye wikiendi iliyopita alikuwa nchini Rwanda kwa ajili ya Shoo ya Instagram Party alisema kuwa, sasa hivi anafanya mazoezi takriban mwezi mmoja, lakini ameanza kuona matunda yake na anajilaumu alikuwa wapi kwa kipindi chote hicho na kushindwa kufanya mazoezi kwani mwili aliokuwa nao usingekuwepo. “Nina mwezi mmoja sasa tangu nianze mazoezi ya kupunguza mwili, lakini ninafurahia maisha haya na najuta kwa nini sikuanza mapema,” alisema Wema.
Stori: Imelda Mtema

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WEMA UTAMDATISHA DOMO TENA.... SHAULI YAKO
    HAMORAPA AMESHAOMBA NAMBA... KINA MANARA PIA WANATAFUTA MSHENGA KUJA NYUMBANI.
    SASA NA MWILI HUU ITAKUAJE SASA????

    ReplyDelete
  2. HIYO NDIYO INAITWA DAYATI HEAVI. UMEPENDEZA KIMWANA.
    HAJI MANALA UKITAKU KULA KATIKA HALAKATI ZA KUGOMBEA ULAISI HAPO UMEZIVUNA ZOTE.
    ISIIACHIE HII DILI.
    HUYU ANAKULA KULIKO ALIZOKUWA NAZO EDO.
    UTAAPISHWA TUU NA MADAMU.

    ReplyDelete
  3. HIYO NDIYO INAITWA DAYATI HEAVI. UMEPENDEZA KIMWANA.
    HAJI MANALA UKITAKU KULA KATIKA HALAKATI ZA KUGOMBEA ULAISI HAPO UMEZIVUNA ZOTE.
    ISIIACHIE HII DILI.
    HUYU ANAKULA KULIKO ALIZOKUWA NAZO EDO.
    UTAAPISHWA TUU NA MADAMU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad