Sumaye: Hatuwezi kukubali CCM iendelee kutawala nchi wakati watu wanazidi kuwa na hali mbaya ya maisha

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Frederick Sumaye ambaye kwa sasa ni mwanachama wa CHADEMA, amesema upinzani hauwezi kukubali kuacha CCM iendelee wakati hali ya maisha ya watu inaendelea kuwa mbaya.

Sumaye ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye mkutano Kimara jijini Dar es salaam alipokuwa akimnadi mgombea udiwani wa CHADEMA, na kusema kwamba hali ya uchumi na maisha ya wananchi kwa sasa ni mbaya zaidi, lakini iwapo wakisema ukweli wanaonekana ni waongo hivyo sio suala la kuendelea kulifumbia macho na kuacha CCM iendelee kutawala.

"Hatuwezi kukubali CCM iendelee kutawala nchi hii wakati watu wanazidi kuwa na hali mbaya ya maisha, tukiwaambia watu wana hali mbaya wanasema tunasema uongo, tukisema uchumi umezama wanasema tunasema uongo, kama tunasema uongo kwa nini hali za wananchi zinakuwa mbaya, maana kuna vitu ambavyo havijifichi, kama uchumi unakwenda vizuri tafsiri zake itaionekana kwenye hali ya wananchi, hali ya wananchi ni mbaya", amesema Sumaye.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya vyama vya upinzani kudai kuwa uchumi wa nchi umeshuka, huku serikali ikikanusha na kuoa taarifa kuwa suala hilo halina ukweli wowote, kwani uchumi wa nchi umetengemaa kutokana na kubana matumizi.

Credit: EATV
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lol huyu naye Lmfao. Mmmmm si upoteee tu katika hizi midia wala huna jipya michosho tu. chefuuu hadi anatuchefuaa hapaa

    ReplyDelete
  2. Wapi Mr. Zero Brain......hebu tuambie, enzi za uwaziri mkuu wako mambo yalikuwaje?? Tangu nizaliwe mpaka sasa ni'muhenga, huu msamiati wa 'hali-ngumu' haujabadilika, iweje leo jumba bovu mnalisukumia kwa JPM?? Nyie wezi na mafisadi wa mali ya uma, hebu mumpumzishe huyo mzee wa HAPA-KAZI-TU, ana moyo hana jiwe, mengine msimsingizie mfyuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad