Takukuru Yamsaka Mgombea wa Uenyekiti CCM Mkoa wa Mara

Takukuru Yamsaka Mgombea wa Uenyekiti CCM Mkoa wa Mara
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imetangaza kumsaka mmoja wa wagombea uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara kwa mahojiano akituhumiwa  kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Wanachama wa CCM wanaowania uenyekiti katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 3,2017 ni Msuto Chirangi, Thobias Raya na Samuel Kiboye, maarufu Namba Tatu.

Akizungumza kwa sharti la kutomtaja jina hadi atakapotiwa mbaroni, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara, Alex Kahunda amesema taasisi hiyo pia inawasaka wanachama wawili wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wanaodaiwa kuwa mawakala wa mgombea huyo wanaodaiwa kuzunguka kugawa rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.

Awali, Kahunda aliwaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM unaofanyika mjini Musoma leo Jumatano Novemba 29,2017 kuwa taasisi hiyo inafuatilia nyendo za wote wanaowania uongozi ndani ya CCM na jumuiya zake.

Ameonya kwamba yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa ataishia mikononi mwa maofisa wa Takukuru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad