TANESCO yatekeleza Agizo la Rais Magufuli, Yaanza Kubomoa Jengo Lake

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza hatua ya ub0omoaji kwenye sehemu ya jengo lake kama utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli  alilotoa mwanzoni mwa mwezi huu ili kupisha ujenzi wa daraja la juu la ubungo.



Soma taarifa iliyotolewa na Tanesco kwa Vyombo vya Habari leo Novemba 27, 2017.

“Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa TANESCO imeanza utekelezaji wa  Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa  kwa Jengo la Ofisi za TANESCO Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam. Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa, pia  baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama  zaidi. Uongozi wa Shirika   pamoja na Wakala wa Majengo TBA wanaendelea kufanya taratibu zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa Shirika. Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais. Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya manunuzi ya LUKU. Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea.”

Mapema mwezi huu Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati akikagua ujenzi wa daraja la ghorofa tatu barabara ya Ubungo, aliamuru sehemu ya jengo la TANESCO na jengo la Idara ya maji kwenye eneo la barabara kuvunjwa ili kupisha ujenzi huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad