Umoja wa ulaya umeipatia Tanzania jumla ya Euro Million 50 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 129 za kitanzania katika kufadhili Mpango wa Taifa wa umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji elfu 12 vitapatiwa umeme
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutia saini juu ya ufadhili huo wenye masharti nafuu ambapo Tanzania haitatakiwa kurejesha Fedha hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bwana Dotto James amesema kuwa umoja waulaya unalenga kuona mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5 unafikiwa kikamilifu hususani katika sekta ya nishati katika uzalishaji na usambazaji ili kurahisisha shuguli za kimaendeleo nakuondoa umasikini vijijini
Kwa upande wa Kamishna wa Umoja wa Ulaya Duniani Mr. Neven Mimica anasema, kufikiwa kwa mpango wa tatu wa umeme vijini REA unaomalizika 2020 kunategemea upatikanaji umeme wa uhakika suala ambalo litachochea kwakiasi kikubwa kufikiwa kwa mpango wa maendeleo endelevu ya dunia ya mwaka 2025
Ufadhili wa maendeleo ya umoja wa ulaya kwa Tanzania kwa sasa unafikia jumla ya Trillion I .07
Honger Watanzania Na hongera kwa Pres JPJM Na Team yako Na utensaji bora Na ufatiliaji bora mpaka mataifa ya njr yanajua kuwa hela hizi hazitoliwa wakati juu WA awamu ya Bulldozer.
ReplyDeleteYou play �� you are fired.
Magufuli has changed the game.
Its no longer business as usual