Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Kidao Wilfred limetoa ufafanuzi ya tuhuma zilizoenea mitandaoni juu ya kashfa ya kulipana posho za mamilioni ya fedha.
Wilfred kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesema kuwa amewasiliana na rais wa TFF, Wallace Karia na kumpatia kibali cha kuzungumzia juu ya jambo hilo.
“Kikubwa nilichowaitia hapa kwa sikumbili hizi kumekuwa na habari zimesambaa kwenye mitanao ya kijamii ikiishutumu uongozi mpya wa TFF kwamaana ya kulipana viwango vya posho, maswala ya mishahara na mambo mengi.” Amesema Kidao
Kidao Wilfred amesema “Naamini kuna watu watakaochukia kwa hizi hatua tunzochukua, lakini hatuwezi kurudi nyuma kwenye hili, hakuna aliye juu ya sheria. Lazima, kama mwanahabari uwe na uhakika na unachokiandika, hauwezi kukurupuka tu.” Kidao.
Kaimu Katibu huyo amesema, ni lazima utamaduni wa kuongoza mpira ndani na nje ya TFF ubadilike.
“Hivyo, baada ya kikao hiki mwanasheria wetu atakwenda kuwaripoti kwenye vyombo husika watu wote waliokuwa wanasambaza taarifa hizi za uongo na kuchafua sura ya TFF,”
“Tayari tuna majina 10 ya watu ambao walikuwa wanasambaza taarifa hizi za uongo na kutuchafua kinyume kabisa na Sheria ya Mitandao. Tunataka wakathibitishe tuhuma hizi kwenye vyombo vya dola,”.
Taarifa iliyokuwa inasambaa mtandaoni ni pamoja na
Kamati ya utendaji ya TFF imeongeza posho za vikao tofauti na hapo awali
Wajumbe wa kamati ya utendaji kilammoja kulipwa shilingi milioni moja.