Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ameitaka Kampuni ya Mkonge ya China State Farms Agribusiness, inayofanya kazi zake mkoani Morogoro kuhakikisha inatoa mikataba inayotambulika kwa watumishi wake.
Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo alipotembelea kiwanda cha Mkonge cha kampuni hiyo kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, baada ya kuapata malalamiko ya watumishi kukosa mikataba pamoja na kuwa wametimiza vigezo.
Baada ya kutembelea kiwanda hicho Dkt. Tizeba alipata nafasi ya kuonanan na wafanyakazi ambao walimweleza kero zao ambazo ni pamoja na mishahara duni, ukosefu wa mikataba na mazingira magumu ya kazi.
Kwa upande mwingine Waziri Tizeba, amewataka wawekezaji wa zao la Mkonge kutumia teknolojia itakayotoa faida zaidi na kuleta tija katika zao la Mkonge nchini sambamba na ukuaji wa pato la taifa kupitia zao hilo.
Katika mfululizo wa ziara zake mkoani Morogoro wazir Tizeba pia amepata nafasi ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mkunazi 2 na kuwataka wawekezaji wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa uendeshaji wake hautaongeza bei ya Sukari bali utoe ahueni kwa wananchi wa hali ya chini kuweza kumudu bai za sukari.
Tizeba Ameagiza Kampuni Kutoa Mikataba Inayotambulika
0
November 22, 2017
Tags