Toleo bandia la programu ya huduma ya kutuma ujumbe ya WhatsApp lilipakuliwa zaidi ya mara milioni moja kutoka kwa programu ya Google Play Store kabla ya kuondolewa.
Programu hiyo kwa jina Update WhatsApp Messenger ilionekana kutengezwa na kampuni ilioanzisha huduma hiyo WhatsApp Inc.
Kulingana na watumiaji katika mtandao wa Reddit, huduma hiyo bandia ilikuwa na matangazo na ilikuwa ikipakua programu hiyo kwa vifaa vya watumiaji wake.
Tofauti iliokuwepo ilikuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kutambua.
Watumiaji ambao walipokea programu imara ya huduma hiyo hawakuathiriwa.
Sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Google kulazimika kuondoa programu feki katika hifadhi yake ya Play Store.
Mwaka 2015, kampuni hiyo ililazimika kuingilia kati na kuifunga programu moja iliojidai kutathmini betri na ilikuwa ikituma ujumbe wa maandishi katika simu za wateja.