Trump na Xi Waanza Mazungumzo Baada ya Makaribisho ya Kifahari

Trump na Xi Waanza Mazungumzo Baada ya Makaribisho ya Kifahari
Rais wa Marekani Donald Trump ameanza mazungumzo na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing kufuatia makaribisho ya kkifahari katika mjihuo wa taifa hilo.
Bwana Trump anatarajiwa kuzungumzia kuhusu vile China inaweza kukabiliana na mipango ya kinyuklia ya Korea Kaskzini swala amblo litatawala ziara yake ya rasi ya Korea.
Marekani inaitaka China ,ambaye ni mshirika mkuu wa Pyongyang kuishinikiza zaidi lakini Beijing imesema kuwa imefanya ya kutosha.
Viongozi hao wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani pia wanatarajiwa kujadiliana kuhusu mapungufu yao ya kibiashara .

Mapema katika zaira hiyo ya mataifa matano, bwana Trump aliitaka Korea Kaskazini kuingia mkataba ili kumaliza mipango yake ya utengenezaji wa silaha za kinyuklia, huku pia akiionya dhidi ya uchokozi zaidi dhidi ya Marekani na dunia nzima , akisema ''musitujaribu''.
Pia ameitaka China kufutilia mbali ushirikiano wao na Pyongyang na kusisitiza wito wa Beijing kulishinikiza taifa hilo.
China imesema kuwa inafanya kila iwezalo na kusisitiza kuwa inatekeleza vikwa vya Umoja wa matiafa kwa ukamilifu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad