Twitter Yafanya Mabadiriko Yawaruhusu Watu Wengi Kutumia Tarakimu 280 Kuandika Ujumbe

Twitter Yafanya Mabadiriko Yawaruhusu Watu Wengi Kutumia Tarakimu 280 Kuandika Ujumbe
Twitter imetangaza kwamba imeanza kuwafungulia watu wanaoutumia mtandao huo wa kijamii uwezo wa kuandika ujumbe kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140.
Kampuni hiyo ilikuwa imewawezesha baadhi ya watu kutumia tarakimu hizo lakini kwa majaribio tangu Septemba.
Lakini sasa wamesema watu wengi wataruhusiwa kuandika ujumbe mrefu.
Watakaozuiwa pekee ni wale wanaoandika ujumbe kwa Kijapani, Kichina na Kikorea ambao wanaweza kuwasilisha maelezo zaidi kwa kutumia tarakimu chache.
Twitter wamesema majaribio yalifanikiwa.
Mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango wa Twitter kuwavutia watu zaidi.
Wakati wa majaribio, ni ujumbe 5% ambao ulikuwa na urefu wa zaidi ya tarakimu 140 na ni 2% uliokuwa na zaidi ya tarakimu 190, wamesema.
Lakini walioandika ujumbe mrefu walipata wafuasi zaidi, walihusiana na watu zaidi na walitumia muda zaidi katika mtandao huo.
"Tuliona kwamba watu walipohitaji zaidi ya tarakimu 140, waliandika ujumbe kwa urahisi na mara nyingi. Muhimu zaidi, watu waliandika ujumbe wa chini ya tarakimu 140 mara nyingi zaidi na ufupi wa ujumbe wa Twitter ulisalia," meneja wa bidhaa na huduma wa Twitter Aliza Rosen ameandika.
Mabadiliko hayo yalipotangazwa mara ya kwanza, wengi waliyakosoa na kusema badala yake wangelipenda kuona taarifa za chuki pamoja na mashine zinazoandika ujumbe zikidhibitiwa zaidi.
Aidha, wengi walitaka ujumbe urudi kufuata historia tena, ujumbe wa karibuni zaidi ukionekana mwanzo na pia waweze kuhariri ujumbe.
Mtandao huo kwa sasa una watu 330 milioni, idadi ambayo ni ya chini ukilinganisha na 800 milioni wa Instagram na zaidi ya 2 bilioni wa Facebook.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad