Ukomo wa Mifuko Mitano Tanzania Bara ni Machi, 2018; PSPF na NSSF pekee kubaki

Ukomo wa Mifuko Mitano ni Machi, 2018 na Mifuko miwili kuimarishwa au kudumishwa na ambapo idadi ya wanachama, madeni, makesi au madudu yeyote kutoka mifuko mitatu hiyo kukabidhiwa kuridhiwa na mifuko miwili yaani PSPF na NSSF. Kwani Tarehe 6 Novemba 2017 mifuko hiyo mitatu imepewa amri ya kupeleka idadi ya wanachama, mali zote, madeni na makesi zote kwa utayari wa umiliki.

Sasa utitili wa mifuko Tanzania Bara sasa unafikia kikomo ambapo SSRA atapumua na kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi kuanzia Mwezi wa Machi 2018 kutoka mitano (PSPF, NSSF, PPF, LAPF na GEPF) kufikia miwili kwani awamu ya Tano imefanya maamuzi magumu na yenye busara kabisa.

Awamu ya Nne ya Jakaya ilikuwa na huo mpango wa kuunganisha mifuko lakini zoezi lilikuwa linasusua kwa safari zake Mzee wa Kaya kwenda Ulaya kila kukicha.

Kuna sekta mbili ambapo mifuko miwili itaimalishwa na mitatu kumezwa. Mfuko wa PSPF utachukua wanachama wote wa public sector kutoka mifuko ya PPF, GEPF na LAPF.

Mfuko wa NSSF utachukua wanachama wote wa private sector kutoka PPF, GEPF na LAPF. Wakati NHIF itaendelea kusajili wanachama kutoka public na private sector pasipo kikwazo cha umri na utaendelea kupata huduma ya kiafya mpaka ukomo wa maisha yako.

Angalia mchakato wa Chati.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad