Uteuzi wa Dr. W.P.Slaa kuwa Balozi: Rais Magufuli Anaendelea Kujieleza na Kujipambanua Kisiasa

Mwanzo mwanzoni nikiri kuwa nimefarijika sana kwa uteuzi wa Dr. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi. Uteuzi huo umefanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli. Nimefurahi kwakuwa Dr. Slaa, kwa weledi wake, usomi wake, kwa sifa zake uzoefu wake na ubobezi anastahili uteuzi huo au wowote kwa ajili ya kuitumikia nchi.

Kwa uteuzi wa Dr. Slaa kuwa Balozi, Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anaendelea kujieleza na kujipambanua. Anajipambanua kuwa anasimamia kauli zake. Mara kwa mara hutamka kuwa 'maendeleo hayana chama'. Na akawahi kukaririwa akisema kuwa anaweza kumteua hata asiye mwanaCCM kama tu ana sifa. Akafanya hivyo kwa Mama Mghwira na kwa Prof. Kitila Mkumbo.

Teuzi zake nje ya CCM, pamoja na kwamba zinaweza kuzua malalamiko, manung'uniko na maumivu kwa wanaCCM, zinajieleza na kujipambanua kuwa uwezo, uzalendo na uchapakazi ndiyo vigezo pekee vilivyobaki katika teuzi za Rais Magufuli. Kwake yeye, hakuna tofauti kati ya mwanaCCM au mwanachama wa chama kingine au asiye na chama kama Dr. Slaa. Ipso facto,Mr. President depicts himself.

Ndiyo maana, katika moja ya michango yangu humu, nimewahi kusema kuwa Rais Magufuli ni 'Jenerali wa Kisiasa'. Anachofanya ni kukusanya na kushambulia tu katika kusimamia ajenda zake alizoahidi na anazoziahidi.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alijitoa chadema .sasa wote wakishajitoa wanakuwaga Chama gani? Amechaguwa mtu wa ccm .

    ReplyDelete
    Replies
    1. we kweli zuzu ni wapi alitangaza kuwa amerudi CCM???? acheni kuwawekea maneno mdomoni mfyuuuuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad