Video; Nitakufilisi ya Queen Darleen

Video; Nitakufilisi ya Queen Darleen
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB Wasafi Tanzania, Mwajuma Abdul a.k.a Queen Darleen amedondosha mkono mpya kabisa unaokwenda kwa jina ‘Nitakufirisi’ chini ya utayarishaji wa Producer Laizer Classic katika studio za Wasafi Records.

Ikiwa ni kazi ya pili kutoka kwa Queen Darleen chini ya usimamizi wa WCB Wasafi, baada ya ile ‘Kijuso’ aliyoshirikiana na Rayvanny. ‘Nitakufirisi’ umetimiza ahadi ya Queen Darleen iyotoka katikati ya mwaka huu katika mahojiano na Dizzim Online kuwa mwishoni mwa mwaka huu ataanza kuachia kazi zake rasmi.
Hata hivyo Queen katika ngoma hii mpya ameuzungumzia mfumo na hali ya kimahusano wa akina dada(kwa kuuvaa uhusika) na wanaume wenye kuiamini nguvu ya pesa katika kujiridhisha kimapenzi kwa kuwapa jibu kuwa kwa mwendo huo atawafirisi ‘Nitakufirisi’.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad