VIDEO:Rais Magufuli Akisikiliza Wimbo wa Kisukuma na Mama na Dada Yake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anasikiliza wimbo wa kabila la wasukuma pamoja na Mama yake mzazi, Suzana Magufuli na Dada yake Mkubwa Monica Joseph Magufuli.

Rais Dkt Magufuli yupo mapumzikoni kijijini kwake Lubambangwe, Chato Mkoani Geita.

Aidha, Rais anatarajia kufanya ziara Mkoani Kagera kuanzia tarehe 06 hadi 09 Novemba, 2017.

Dhumuni la ziara ya Mhe. Rais Magufuli ni kuwatembelea wananchi wa Mkoa wa Kagera pia kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani hapa.

Vilevile  Mhe. Rais Magufuli atapata fursa ya kuongea na wananchi  kwenye Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa yeyote anayehusika, hivi ni lini mara yako ya mwisho kumtembelea mama yako mzazi, sio kumpigia simu, kumtembelea....hongera sana Prezidaa, pamoja na kazi ngumu ya 'kuinyoosha' TZA, bado unapata nafasi ya kumtembelea mama yako mzazi,,,,sishangai kwa nini mambo yanakunyookea, yote ni baraka za wazaza, hasa MAMA......Mungu akubariki sana, AMEEN

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad