Vifo vya MANGULI vilivyozua Utata, Lakini Hadi Leo Havijapatiwa Ufumbuzi…

1. Christopher Wallace (Big Small)

Alikuwa ni mwanamuziki maarufu wa miondoko ya Rap nchini Marekani. Ni takriban miaka 20 tangu auawe lakini mpaka sasa bado kifo chake kimebaki kuwa kitendawili kigumu kwa Polisi wa Los Angeles. (LAPD). Wengi wanaamini kwamba Suge Knight alihusika na mauaji ya Biggie lakini LAPD walikataa kumhoji Suge au hata kumhoji mtu yeyote kuhusiana na mauajai hayo.

Hadi leio haijulikani ni nani alimuuwa rapa huyo kutoka viunga vya Brooklyn.


2. Tupac Shakur:

Je inawezekana kundi la Christopher Wallace (Biggie) lilihusika na mauaji ya Tupac Shakur mnamo mwaka 1996? Hapana. Hakuna anayejua hasa ni nani alifyatua risasi ambazo zilikatisha uhai wa Tupac. Watu wengi hawaamini kama Tupac amekufa. Hata hivyo baada ya kifo chake zilikuja kutolewa album zake 6 ambazo alizirekodi lakini zilikuwa bado hazijaingizwa sokoni.



3. Yaki Kadafi:

Miezi michache baada ya kifo cha Tupac, mtu pekee aliyeshuhudia tukio la kuuawa kwa Tupac naye aliuawa. Akiwa amejipumzisha nyumbani kwa mpenzi wake, mtu asiyefahamika alibisha hodi na Yaki alimkaribisha. Alipoingia alimmiminia risasi na kutoweka.

Cha kushangaza hadi leo hii hakuna anayefahamu ni nani alihusika na mauaji ya Yaki Kadafi.


4. Princess Diana:

Hivi ni kweli Princess Diana alikufa kwenye ajali wakati akiwakimbia waandishi wa habari maarufu kama paparazzi? Au Familia ya kifalme ilitengeneza hiyo ajali ili kukatisha ndoa yake na kijana wa Kiislamu Bilionea Dodi Al-Fayed na kuzaa naye mtoto. Kamwe hakuna anayejua ukweli kuhusu kifo cha mwanamke huyu. Lakini labda tusubiri matokeo ya upelelezi mpya kuhusu tukio hilo ambao huenda ukafumbua kitendawili cha kifo cha Princess Diana.


5. Jimi Hendrix:

Je kifo cha Jimi Hendrix kilichotokea mwaka 1970, kilikuwa ni cha kupangwa au ni ajali? Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi wa kifo chake, ilidai kwamba, Jimi alipaliwa na matapishi yake yaliyotokana na ulevi. Lakini pia taarifa hiyo ilibainisha kwamba mapafu yake yalikutwa yakiwa na mchanganyiko wa mvinyo na dawa za kupunguza msongo wa mawazo (Barbiturates). Lakini baadhi ya watu wanaamini kwamba meneja wake Mike Jeffery ndiye aliyemuua kwa kumchanganyia hicho kinywaji.



6. Jason William Mizell:

Mnamo mwaka 2002 mtu asiyefahamika aliingia katika studio ya Queens na kumkumbatia (Hug) Jam Master Jay na kummiminia risasi. Baadhi ya watu walidai kwamba mtu huyo anahusiana na Tajiri mmoja wa madawa ya kulevya aitwaye Kenneth "Supreme" McGriff ambaye alitaka Jay auawe kwa sababu ana uhusiano wa karibu na 50 Cent. Lakini hakuna yeyeote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo la mauaji ambalo lilitikisa jamii ya wanamuziki wa hip hop nchini Marekani.

[​IMG]

7. Elvis Presley:

Kwa mujibu wa uchunguzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya inayohusika na vifo visivyo vya kawaida (Coroner),Elvis alikutwa na umauti akiwa chooni baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi ghafla kutokana na kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya. Lakini ukimuuliza shabiki yeyote wa Elvis atakwambia mtu huyu bado yu hai. Huenda wako mahali wametulia yeye na Tupac.



8. Natalie Wood:

Wakati muigizaji maarufu nchini Marekani Natalie Wood alipokutwa akiwa amekufa maji umbali wa maili kadhaa kutoka ilipo mashua yake hapo mnamo mwaka 1981, mamlaka ya kisheria nchini humo iliamini kwamba Natalie alikuwa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya ndipo labda akateleza na kuzama majini na hatimaye kufa. Lakini kulikuwa na watu wengine wawili ndani ya boti hilo. Minong'ono inadai kwamba Natalia alikuwa na uhusiano wa siri na Christopher Walken ambapo mumewe aitwae Robert Wagner alikasirishwa na jambo hilo ndipo akamuuwa. Mpaka sasa si Christopher Walken wala Robert Wagner aliyepata kuzungumzia tukio hilo.

[​IMG]

9. Patrick Lamark Hawkins:

Mnamo Februari 1998 mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya Rap wa Houston aitwae Fat Pat aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa Promota wake. Mauaji hayo yaliishtua mashabiki na jamii ya wanamuziki wa Rap nchini Marekani.

Lakini hadi leo aliyehusika na mauaji hayo hajakamatwa. Lakini hata hivyo inaaminika kwamba muuzaji maarufu wa madawa ya kulevya katika eneo hilo aitwae "Weasel" aliamuru Fat Pat auawe. Mauaji hayo yalihusishwa na matukio ya ujambazi katika eneo hilo.



10. Bob Marley:

Taarifa rasmi zinadai kwamba Bob Marley alikufa kwa ugonjwa wa Saratani (Cancer). Lakini rafiki wa karibu wa Bob aitwaye Lee Lew Lee alidai kwamba, kuna mtu alimtegeshea sumu ya kemikali ambayo ndio iliyo sababisha kifo chake. Kansa iliyoanzia katika dole gumba la mguu wake ndiyo iliyochukua uhai wa nguli huyu. Kansa hiyo ilitokana na kuumizwa na kipande cha chuma aina ya shaba ambacho Lee alidai kilipachikwa kiufundi ndani kiatu chake kilichonunuliwa na kukabidhiwa kwa Bob Marley muda mfupi kabla ya kuingia uwanjani.

[​IMG]

11. Anna Nicole Smith:

Kifo cha mwanamke huyu kimejaa utata mtupu. Mwaka 2006 mwanaye wa kiume alifariki kutokana na kutumia kiwango kikubwa cha dawa. Miezi sita baadaye Anna naye likufa kutokana na aina ya mchaganyiko wa dawa ambao ndio uliomuuwa mwanaye. Wengi wanajiuliza, Je inawezekana Anna ameamua kujiua mwenyewe kwa mchanganyiko huo wa dawa au kuna mtu alimtengenezea huo mchanganyiko wa dawa ili kummaliza….?



12. JonBenet Ramsey:

Niliwahi kuandika kuhusu mauaji ya binti huyu hapa JF: kwa kujikumbusha unaweza kubofya hapa: https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/279017-jonbenet-ramsey-mauaji-yake-yalikuwa-ni-ya-ajabu-3.html

Kesi hii ambayo mpaka leo hii haijapatiwa ufumbuzi na FBI, ilijizolea umaarufu si nchini Marekani pekee bali pia ulimwenguni kote. Pengine unaweza kushangaa inakuwaje nchi kama Marekani ambayo inatisha kwa upelelezi lakini inashindwa kupata ufumbuzi kwa kesi hii ambayo mauaji yake yaliacha maswali mengi sana yasiyo na majibu. Binti huyu aliuawa usiku wa Disemba 1996 akiwa na umri wa miaka 6 wakati huo.

Wazazi wake waliripoti binti yao kupotea, lakini masaa nane baadaye alikutwa akiwa ameshakufa. Mwili wake ulikutwa katika chumba kilichokuwa ghorofa ya chini(Basement) hapo nyumbani kwao. Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji yake, lakini wazazi wake mpaka sasa wameendelea kuwa miongoni mwa watuhumiwa kuhusiana na mauaji hayo, takriban miaka 20 tangu kuuawa kwake.



13. Marvin Gaye:

Kila mtu anajua kwamba Marvin Gaye aliuawa kwa kupigwa risasi na baba yake. Lakini wengi wanajiuliza kwamba, je ilikuwa ni mauaji au ni kitendo cha kujiuwa? Inadaiwa kwamba, Marvin alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio yalipotokea mauaji. Hivyo alimuomba baba yake amuue baada ya yeye kushindwa kujiuwa mwenyewe. Kwa mujibu wa matamshi yaliyotoka kinywani mwake baada ya kupigwa risasi na baba yake, alisikika akimweleza kaka yake aitwae Frankie kwamba:

"Nimepata kile nilichotaka.. Sikuweza kufanya mwenyewe hivyo nilimuomba yeye afanye hivyo badala yangu. Ni vizuri kwamba naondoka na hakuna kilichobaki nyuma yangu…"

14. Shakir Stewart:

Def Jam Executive VP Shakir Stewart alikuwa ni moja ya nguzo za Def Jam. Kwani akiwa ndiye Executive VP wa Def Jam aliwahi kuingia mikataba na wanamuziki maarufu nchini marekani wakiwemo Young Jeezy, Rick Ross na Beyonce.

Mnamo Novemba 1, 2008 Shakir Stewart alikutwa ndani ya bafu katika nyumba yake iliyoko Atlanta akiwa amekufa. Alikutwa akiwa na jeraha la risasi aliyopigwa kichwani. Kwa mujibu wa uchunguzi, ilidai kwamba, Shakir alijiuwa mwenyewe kwa kujipiga risasi.

Hata hivyo marafiki na familia yake walidai kwamba, kundi la Mafia ndilo lililomuuwa na kutengeneza mazingira ili kuonyesha kwamba Shakur amejiuwa mwenyewe
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watu wasio Julikana ni wageni Tanzania tu. Lakini nchi kama Marekani ni matukio ya asili Kwani hata akina Kenedy brothers vifo vyao wauaji halisi mpaka Leo kujulikana ni kizungu mkuti.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad