Wafanyakazi Watangaziwa Kiama

Wafanyakazi Watangaziwa Kiama
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew John Mtigumwe amesema kuwa asilimia kubwa ya maafisa ugani nchini hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao.

Ameyabainisha hayo wakati akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata ya Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.Kutokana na kubaini hilo Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa Wizara ya kilimo inaandaa utaratibu wa kuwarudisha shule maafisa ugani ambao elimu zao ni ndogo na zimeshindwa kukidhi mahitaji ya wakulima.

Aidha katibu huyo mkuu amebainisha kuwa maafisa ugani hao watafanyiwa usaili upya ili kubaini uwezo wao kwani wengi wao wameajiriwa na serikali lakini wakulima hawanufaiki na elimu.Pamoja na hatua hizo katibu ameeleza kuwa maafisa ugani ambao wataonekana kushindwa kabisa kufikia vigezo na kuwa msaada kwa wakulima basi wizara itapendekeza waondolewe kazini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad