Wakurugenzi, Watumishi Kukatwa Mishahara

Wakurugenzi, Watumishi Kukatwa Mishahara
Katibu mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro amewataka wakurugenzi, wakuu wa idara na watumishi wote kuwa wazalendo na kuwatumikia vyema wananchi.

Katibu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa manispaa ya Songea, ambapo ameeleza kuwa, ni lazima kila mtumishi atimize majukumu yake ili kurahisisha majukumu ya mwingine kwani idara nyingi zinategemeana kiutendaji.
“Kila mtumishi inabidi ajitathimini abadilike awe mwadilifu zaidi, awe mchapakazi zaidi, awe binadamu zaidi na awe mwaminifu zaidi”, amesema Ndumbaro.
Aidha Dkt. Dumbaro amewataka Wakurugenzi na Maafisa utumishi kushughulikia na kuyatatua matatizo ya watumishi na endapo hawatafanya hivyo basi wizara itasimamisha mishahara yao ili nao wapate usumbufu kama wanaopata watumishi wa kawaida.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad