Wanachadema 12 Wakamatwa kwa Kumshambulia Diwani Arusha

Wanachadema 12 Wakamatwa kwa Kumshambulia Diwani Arusha
Siku kadhaa baada ya wanachama 12 kutoka Chadema kukamatwa kwa kosa la kumshambulia mgombea wa udiwani wa kata ya Muriet wilayani Arusha, Francis Mbise wanatarajiwa kupandishwa kizimbani leo.

Wafuasi hao akiwemo Kaimu Katibu wa Chadema wilayani Arusha, Innocent Kisanyage walishikiliwa  na polisi eneo la FFU kwa Morombo wakidaiwa kumshambulia mgombea huyo wa CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Novemba 5 Kamanda  wa Polisi jijini Arusha (RPC), Charles Mkumbo alisema kwamba wafuasi hao wote 12 watafikishwa mahakamani leo Jumatatu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad