Wanachama 50 wa CHADEMA Wahamia CCM

Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Vijana  hamsini wanachama wa CHADEMA kutoka kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw. Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.

Katika kampeni hizo  Bw. Rajab amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ujumla kwani bila kufanya hivyo .

Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye wamemsimamisha.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapi Nassari?? Na hao wamenunuliwa ama nene?? Mtajutraaaaaaaa.......HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Its more complicated than that. Wengi wajinga.

      Delete
  2. Wasukuma hao. Wakaskazini hao. Waache wahame hawajui watendalo. Wanamuunga mkono mwenzao. Lakin nawahakikishia Watanzaia. Chadema ni chama pekee kwa sasa nchini chenye misimamo safi, yenye uwezo wa kuleta maendeleo nchini.Ni chadema pekee ambacho viongozi wake wanania njema kuwatumikia wananchi Tanzania na si kulazimisha watanzania. Ni Chadema pekee ambacho wengi wasomi wako na imani na chama hicho. Ni chadema pekee kinaupeo wa kweli wa kuona na kuwasikiliza Watanzania. Wengi wansohama kutoka chadema ukiwsfuatilia kielinu ni shida. Wanamfuata raisi badala ya wao wenyewe kujikomboa. Wanamtegemea raisi awabadilishe badala yso wenyewe kijielimidha, kujituma, na kujikomboa kifikra. Hawana mdimamo na wsnamtegemea bulfoza awape maendeleo badala yso wenyewe kujua ni wao ndio wanahitajika kukiletea maendeleo. Wanaona ndugu Pombe kawaletea uwanja wa ndege, na kuwafanyia mambo mengi huko ndio maana wanahama. Hawajui kama kuna dalili ya upotodhsji kiuongozi.sioni kama ndugu pombe ameweka jitihada sawa kwenye mikoa mingine hasa kudini na magharibi , pwani. Hahudumii watanzania wote sawa. Kuna kiupendeleo fulani. Namuunga mkono Msigwa aliyoyazungumza na yanajidhihirisha wazi. Ukabila na ukanda umeingia na uchsma. Kama uko vhadema jimbo lako haliungwi mkono sawa na jimbo la ccm ingawa majimbo mengi chini ys chadema kiuchumi ysko mbele ccm inachukua malipo ya kodi kuhamishia kwingine na huu ni ubaguzi na ukandamizaji. Anawafanya watu wahamie ccm ili awajali kajisahau kachaguliwa na watanzania . Ni ubinafsi, ucchama, na propaganda anazotumia kuchumia watu. Zitakwisha tu.

    ReplyDelete
  3. Chadema ni chama cha kibuguzi kuanzia mfumo wake hadi matamshi yao. Na kama watanzania wasipokuwa makini na siasa za chadema basi nchi namba moja inayosifiwa barani Africa kuwa na umoja ulioshikana miongoni mwa watu wake utabakia historia tu kipindi kifupi kijacho. Kuna Mcenge hapo juu Kajigamba kabisa kuwa chadema ni chama chenye msimamo safi Tanzania? Lakini ukisoma maoni yake utagundua yakwamaba kweli ni mwanachadema halisi kwani kama kawaida ya chama cha chadema na wafuasi wake siku zote ni kuhibiri ukabila na ukanda. Mambo ya usukuma na ukaskazini hayawezi kuzungumzwa na mtanzania halisi hata afikwe na jazba ya kiasi gani. Mambo hayo ya ukabila huzungumzwa na wapumbavu wakitanzania walioelekeza nguvu zao katika siasa za kikanda na ukabila nchini kitu ambacho ni cha kulaniwa na kila mtanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wasio na akili hawataweza kufikiri. Walaza Akili Tanzania ni wengi mno. Hakuna watu walio na maneno matamu midomoni kama CCM. Nchi hii imeliwa na Wanaccm lakini nawashangaa Watanzania kwa miaka yote hii kuwaachia viongozi wakuu wa CCM huru. Bila kulalamika. CCM inatumbua? mtu mwovu atajitumbuaje mwenyewe. Ataonaje kibazi cha mwingine wakati ana gogo kwenye jicho lake mwenyewe. Kama si siasa chafu, kulindana ni nini. Kwa nini maghorofa ya Lugumi hayauziki. rudini kwenye kesi hizo kuna madingi wa CCM. Ebu acheni siasa chafu nchini za kuhadaa wajinga.Mnazidi kuitumbikiza Tanzania kubaya. Ukiwa na elimu na msimamo ni shida kuwa huru Tanzania .Inabidi uwe mjinga na kondoo. Faida ya elimu ni nini. Mtu msomi bado unadanganya na kulaghai wananchi kwa faida za wachache mkimwacha maskini taabuni. Eti mpo kwa kumsaidia maskini , ni ahadi za Abuwasi za majukwaa kwenye mbwembwe na porojo tupu. Huko ndo mnakowakota hawa wote wanaohamia CCm kwa sasa. Kuvaa kijani ni kinga ya kutokunyanyaswa na polisi, na CCm na utakuwa kipenzi cha raisi. Wee unalala chini kipenzi analala ghorofani. ni kunusa kwa mbali na kucheza ngonjera kwenye majukwaa na hekaluni ili tu uonyeshwe pichani upo kijani, Inferiority complex inaua kichinichin. Aibu.

      Delete
  4. Bado Tanzania iko nyuma sana kifikra. Wengi walio CCM si kwamba wanaamini hata Wanaogopa kupoteza vyeo na kutokuungwa mkono na Raisi Magufuli na CCM. Sijawahi kuona mafisadi nchini kuzidi viongozi wa CCM.Toka tupate uhuru, ni kubadili lugha na kutoa ahadi zisizo na mwisho. Kinaaza vizuri wakati wa uchaguzi na mbwembwe nyingi. Kinapata wajinga wengi sana. Baada ya muda mambo ni yaleyale. Undugu, uchama, ukabila, na uvunjivu wa sheria. Kama Watanzania wengi hata wasomi ni waoga namna hii future ya Tanzania ni matatani. Nilifikiri Wasomi wengi wangedai usawa, uhuru wa fikra na kuchangia mawazo bila kushikwa na polisi. Nilifikiri Wasomi wengi wangedai Katiba kwanza baada tu ya uchaguzi ili watu waongozwe kisheria na viongozi wawe accountable pale wanapovunja sheria bila ya kuwaogopa. Lakini wapi. Woga wa Watanzania wasomi unachagia ujinga wa wasio na visomo kukimbia huku na kule sababu usomi hauwasaidii kufikiri nje ya box. Na hii inatufanya kupiga hatua moja mbele na tatu nyuma kila tuchaguapo viongozi wa CCM. ni mtu mmoja anaamuru mambo na kondoo kuinama vichwa. Inasikitisha sana. No changes baada ya miaka zaidi ya hamsini toka uhuru. Ni manipulation ya CCM , siasa na wanaCCm. Sad.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad