Wasimamizi wa Uchaguzi Wameambiwa Wasitangaze Ushindi wa Wetu Tukishinda- Mashinji

Wasimamizi wa Uchaguzi Wameambiwa Wasitangaze Ushindi wa Chaadema Tukishinda- Mashinji
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda.

Dkt. Vincent Mashinji amesema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya.
"Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda" alisema Katibu Mkuu wa CHADEMA
Mbali hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka.
"JPM kusema wapo watu waliokuwa ni wezi katika CCM na kusema saizi watu hao wamekimbilia CHADEMA. Lazima JPM ajue kuwa “Wameamua kuokoka” Alisema Mashinji.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya maneo ya Huyu Dk Mashinji inaonesha ni jinsi gani Chadema wanavyojua kuwa hawana uwezo wa kushinda mbele ya CCM na kuanza kutoa sababu feki ambazo haziingi akilini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu. Chadema wakishinda wao uchaguzi ni halali na kujigamba wameigaragaza CCM? Lakini wakishinda CCM basi Chadema wameonewa na kudhulumiwa ushindi? Upumbavu wa namba hii kutoka vyama vya upizani nchini tunataka ukome kwani ni aibu na vile vile tabia hii inaweza kuingiza nchi kwenye machafuko kwani upinzani kuwahamasisha na kuwaaminisha wafuasi wao kuwa siku zote chama chao kikishindwa huwa kinadhulumiwa kitu ambacho sio kweli. Tunaamini serikali ya Magufuli ni makini kwa hivyo ingekuwa busara huyu katibu mkuu wa Chadema akathibitisha na kutoa ushahidi wake mbele ya vyombo husika juu ya madai yake haya. Na jambo jengine la fedheha na la kukatisha tamaa ni hili la katibu mkuu wa Chadema Dk Mashinji kukiri yakwamba kweli majizi yanayokimbia kutoka CCM wanakimbilia Chadema kwenda kuokoka? Hivi ni vichekesho na utani katika jambo serious kwenye harakati za kupambana na ufisadi nchini. Tunajua Chama cha chadema sasa ni kama genge la wahalifu wanaotaotafuta utajiri kwa njia ya haramu. Kule Chadema sio kwa kwenda kuokoka bali ni kimbilio na chaka la mafisadi wanaotaka kuendeleza unyonyaji kwa watanzania wanyonge.

    ReplyDelete
  2. Mashinji...!!! Usianzishe Sokomoko.
    Mkisjinda mtapewa.
    Lakini wananchi walivyo eashtumia Na ukanda mno ubavu..???
    Wacheni kujihami.
    Hamna nao mbele ya wananchi Na utendaji WA Magu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad