"Watanzania Watakuwa Vibarua tu" - Zitto

"Watanzania Watakuwa Vibarua tu" - Zitto
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka na kudai kwamba utekelezaji wa miradi kupitia serikali ya awamu ya tano inaharibu uchumi wa nchi bila kujali maslahi ya Taifa na wananchi wake.
Zitto ametoa hayo ya moyoni kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kwamba Mkataba ambao serikali ya awamu ya tano imeingia na Uturuki katika ujenzi wa reli haujawazingatia Watanzania wenye viwanda vya chuma ambacho ni kitu kinachohitajika katika mradi huo wamenyimwa na badala yake wamekabidhiwa kampuni ya Uturuki.
Mh. Zitto ameongeza kwamba Mkataba ambao serikali umeingia na Waturuki hao hauwalazimishi kutumia malighafi za nyumbani ingawa wameingia mkataba wa sh. Triliomi 7.
"Kwa masikitiko makubwa nawaambia Watanzania kuwa Mkataba wa Ujenzi wa Reli waliyopewa kampuni ya Uturuki haukuzingatia maslahi ya Taifa.... . Watanzania wenye viwanda vya kuzalisha Chuma kitu  kinachotakiwa kwenye sehemu ya mradi wamenyimwa kazi hiyo na badala yake kampuni za Uturuki ndio wamepewa kazi hizo. Hata kokoto wamepewa kampuni ya Uturuki. Watanzania watakuwa vibarua tu" . Zitto.
Ameongeza kwamba "Naisihi Serikali itazame hii miradi mikubwa na kuifungamanisha na mkakati wetu wa Viwanda ili kufikia malengo yetu na azma yetu ya kuondoa umasikini nchini kwetu. Hii Serikali ya Awamu ya Tano inaharibu uchumi wetu. Inatekeleza miradi bila kujali maslahi ya nchi yetu. haina maarifa ya kuendesha uchumi,"
Mbali na hayo Mh. Zitto amefafanua kwamba kama nchi ingekuwa na mipango thabiti basi Tanzania ingekuwa wazalishaji wakubwa wa Chuma na na hata uzalishaji wa chuma cha kujengea reli kwenye eneo la Mashariki mwa Afrika na Maziwa Makuu.
"Nchi yetu ina chuma kingi sana kule Mchuchuma na Liganga, na pia tuna makaa ya mawe ya kuchenjua chuma hiki ili kupata chuma cha pua (steel). Mradi huu wa reli peke yake ungeweza kuchochea maendeleo makubwa kwenye sekta ndogo ya migodi na viwanda vya Chuma. Iwapo tungekuwa na mipango thabiti, ".
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Dofo huna laki.
    Sasa unatukera.
    Fatilia Simu laki la kichina huko ulipoliwacha.
    Tena nakeamnieni pamoja Na Udaku.
    Huyu Dogo asituharibie siku katila Blogu yetu.
    Amebaki katika chama Kama mlinzi.
    Wenye ajili zao wamesgaondoka Na CDM walimfukuza.
    Hafai hata kwa aenti ya maji (Ndururu)

    ReplyDelete
  2. Ahaaa... Mfanya biashara.
    Ahaaaa... Mchumi Kilaza.
    Ahaaa....Mwanasherua.
    Ahaaa . .Zitoo Zuber Kabwe
    Mwana Ekti mzalendo..!!;;

    ReplyDelete
  3. Waaahhhhh.... Zitto katoa wazo zuli sana. Tulifanyie kazi.
    sasa ni wizala gani ndiyo husika .
    Zitto Zuberi Kabwe mwana siasa mashuhuli aflika mashariki na kati mpaka kusini na kaskazini kote.
    kutoka katika kitongoji cha kule kwa babu yake Dkt livingistone.
    Umetisha Zitto Zuberi Kabwe Huko Mirembe katika anga zako. Wanakukubali wenzako wote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad