Wazili Mkuu Atoa Majibu Kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya

Wazili Mkuu Atoa Majibu Kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa Changamoto za jamii ni nyingi kuliko mahitaji ya Katiba hivyo suala la katiba sio kipaumbele cha serikali kwa sasa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amefafanua, “Katiba mpya inahitaji gharama kubwa na sisi tumeanza na kutatua changamoto za jamii kwanza, ikiwemo mahitaji ya maji, changamoto za elimu, na sekta ya Afya”. Amesema Waziri Mkuu

Waziri Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo.

“Kila bajeti ina vipaumbele vyake, kwa sasa acha tufanyie kazi vile ambavyo vinasumbua wananchi wengi kwani kipaumbele kikuu ni kuimarisha huduma za jamii hivyo tunasimamia ukusanyaji mapato ili tumalize changamoto hizi na katiba ni muongozo tuu acha tutumie huu uliopo sasa”. Amesema Waziri Mkuu

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu viongozi wa kuu wa CCM.mbajua kwamba nyinyi ni mawakili tu wa watanzania. Navinabidi muacge kufanya kazi kikawaida kama mlivyofanya miaka ya nyuma ba muanze kuwajali, kuwasikiliza wananchi ni nini wamewaomba muwatimizie kwanza .wameomba katiba kwanza ili itoe miongozo safi kwa hayo mnayoyasema eti mnwapa watanzania.kutoa amri juu badala ya kusikiliza chini kwanza kwa watu wsliowachagua ni mfumo wa ubabe na di huru.kila watanzania wanaposema na kukazia tunataka katiba ya warioba mnakwepa na kutoa maneno yabayowarighia nyinyi mkijua kuna wengi watanzania wasio na upeo mnawahadaa kwa maneno matamu na kuwashangilia.huu ni utumiaji mbovu wa madaraka na kukwepa ukweli halisia ni nini watanzania wanahitaji kwanza. Mnalazimisha matakwa yenu kila wakati badala ya kuwa wasikivu wa wananchi na hili linaleta shida kubwa kitaifa. Mnaligawa Taifa na watu bila kumwogopa Munga. Mnachokiogopa ni nini.watu wanadai mnawazima. Je mbatimiza matakwa ya CCM au ya Taifa. Ni migongano kiuongozi ya kichama inayosikiliza ccm na kitaifa au seriksli ambayo watanzania wote kwa pamoja wanahitaji katiba mpya. Mnaweza fanya yote mawili kwa wakati moja. Ebu acheni kulazimisha mambo na badala yake muwe wasikivu na kuto kuwaponda, na kuwadharau watanzania kwa hili.Heshima, na mujibu, utaongozwa na katiba badala ya watu wachache wapendavyo wao.ni upotoshaji mmoja wao na kwa makusudi mazima.kukwepa responsibility na liability.

    ReplyDelete
  2. Katiba ni mwenendo wa maisha yanayo kubalika katika Jamii.
    Kwa Hivi sasa Serikali yetu ya awamu hii ya tano. Tunabana Matumizi yasiyo na Dharura na Kuleta utatuzi wa Adha na kero za maisha kwa Mtanzania za kila siku.
    Na Kuna msukumo mkubwa wa kuboresha na kuanzisha miundo mbinu ambayo itakuwa ni catalyst katima kuanzisha Ajira na kuboresha maingira na maisha ya Mtanzania kumtoa hali ya chini na kumpeleka katika maisha ya kati ambyo moja wapo....ni Elimu/Matibabu / Lishe/ ustawi wa jamii.
    Katiba ni suala ambalo ukifika muda muafaka tutaliangalia lakini siyo ajenda yenye kipaumbele.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad