Waziri Atolea Ufafanuzi Vifaranga Kuchomwa Moto

Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega, ametolea ufafanuzi suala la vifaranga waliokamatwa wakiingizwa nchini kinyume na sheria na kuchomwa moto, na kusema kwamba serikali ililazimu kufanya hivyo.

Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, Waziri Ulega amesema iwapo serikali isingechukua uamuzi huo ingeleta madhara makubwa kwa nchi ikiwemo kuangamiza ndege wafugwao wote na hata kupelekea vifo.

“Mafua ya ndege ni ugonjwa hatari sana tumeshuhudia hapo nyuma nchi zenye maendeleo makubwa zilipata tatizo la mafua ya ndege, watu walikuwa wanatembea wakiwa wamevaa mask, unajaribu kutafakari ikitokea jambo kama hili limetokea kwenye nchi, ina maana ndege wafugwao wote itapaswa waangamizwe, wote, kama kuna mtu ana biashara yake wote wanaangamizwa”, amesema waziri Ulega.

Naibu Waziri huyo aliendelea kwa kufafanua kuwa vifaranga hivyo havikurudishwa kule vilikotoka kama ambavyo baadhi ya watu walikuwa wakihoji, na kusema kwamba muhusika hakuwa na kibali, na iwapo vingerudishwa na kuja kutokea tatizo, lawama zote zingekuwa kwa nchi ya Tanzania.

“Watalam walimuuliza muhusika kama ana kibali akasema hana, na kama hana taratbu ziko wazi, na kuna sheria ambazo zinawaongoza, ukisema umrudishie alafu ikigeuka wakisema vinatoka Tanzania na bahati mbaya ikaonekana vina maradhi na wakautangazia ulimwengu, sisi tungekuwa tumebeba mzigo mkubwa ", amesema Mheshimiwa Ulega.

Naibu Waziri huyo amendelea kwa kusema kwamba inashangaza kwa mtu kuingiza vifaranga kutoka nje ya nchi wakati kuna vifaranga ambao wanazalishwa hapa ndani, na wanakosa soko.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad