Mchezo huo umeweka historia kwa klabu ya Singida United kucheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya miaka 15 kupita ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2012.
Katika mechi za raundi 8 zilizopita msimu huu Singida United walikuwa wakitumia uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Namfua ulikuwa unafanyiwa marekebisho kabla ya Bodi ya ligi kuupitisha rasmi uwanja huo mapema mwezi uliopita.
Katika mchezo wa leo timu zote mbili zimeshambuliana kwa zamu lakini hakuna ambaye alifanikiwa kupachika bao hadi dakika 90 zinamalizika. Eneo la ushambuliaji kwa kila timu walifanya makosa kadhaa huku uimara wa walinda milango Manyika Jr wa Singida na Youthe Rostand wa Yanga kikiwa ndio chanzo kikubwa cha sare ya leo.
Yanga sasa imepaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 17 huku ikisubiri mchezo wa leo ambapo Azam FC yenye alama 16 itacheza na Ruvu Shooting Azam Complex saa 1:00 usiku. Kesho Simba yenye alama 16 itakuwa ugenini kucheza na Mbeya City