Zitto Kabwe Ajipanga Kulishtaki Jeshi la Polisi

Zitto Kabwe Ajipanga Kulishtaki Jeshi la Polisi
Mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe amesema anajipanga kulifunguliwa kesi ya kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.

Zitto ameeleza kuwa Simu yake inashikiliwa tangu 7/11/2017 alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu pamoja na sheria ya makosa ya mtandao.
“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu, nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo”, amesema Zitto.
Kiongozi huyo wa chama cha ACT-Wazalendo ameongeza kuwa, “Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( Cybercrime Act )”.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe zitto na kisomu chako cha kichina umeoona dili.
    Hizo simu kwa wamekusaidia ushukurumungu. si bola ongekuwa nokia ya tochi.
    posho hakuna na unajifanya mwanasmati phoni. TAKWIMU ZAKO NI ZA UPOTOSHAJI KUTOKA HIKO KITEHNO CHAKO.
    NAunua simu ya Hadhi na huko Miremne huwa chinga wanazileta au unataka kwa oda.
    uko wodi namba ngapi ntawambia wakusake huko.
    hapa kazi tu Dogo!!!!
    wako watu wanaota mchana kweupe kulishitaki jeshi letu la usalama kwa raia na wewe mmojawapo. hii spidi huiwezi dogo. wewe kaa pembeni.

    ReplyDelete
  2. zitto umepagawa. wewe uende kumfungulia nani kesi.
    wanachama wamesha kihama kwa tabia zako mbovu.
    una kiranga cha nini.

    ReplyDelete
  3. Zitto Zuberi Kwabwe anatahadharisha Jeshi la polisi kulifikisha mahakamani.
    Kiss na mkasa TELEFONI HAIJALUDISHWA ALIPOIWACHA.
    JE UNAIKUMBUKA JINA NA WASIFU WAKE?

    ReplyDelete
  4. MWENYE cHAMA NA mMILIKI WA aCT IN aCTION.
    ANASISIMKIA JESHI LA POLISI TANZANIA.
    MMEGLESHENI KWA NINI MSIMLUDISHE KULE KWAO??
    WA WAPI HUYU?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad