Zitto Kabwe ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wakewa facebook na kusema kwamba taifa lenye hali kama hii haliwezi kupiga hatua kimaendeleo, hata kama wakijenga miundombinu ya kisasa, na kuitaka serikali kuweka misingi imara kwenye jamii yake.
"Nimepita kituo cha reli ya kati Dar na kuona msururu wa watu. Nimeambiwa wanakwenda kwenye meli ya madaktari wa wachina. Hii ni ishara kuwa watu wetu wanaumwa na hawana uwezo wa kuhudumia afya zao. Taifa lenye hali hii haliwezi kamwe kusonga mbele hata lijenge fly overs kila kona. Maendeleo ni watu, hili liwe somo. Tujenge Hifadhi ya Jamii ya Taifa ili tuwe na Taifa lenye afya bora na Uchumi shirikishi", ameandika Zitto Kabwe.
Hivi karibuni meli kutoka china yenye madktari bingwa imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma ya matibabu kwa wakazi wa jiji hilo bila gharama zozote.
Ama kweli...!!!
ReplyDeleteWewe Zitto Zuberi Kabwe inaiishi Fesi buku.. nasikia hapo bungeni hii si awamu yako ya kwanza.
Je ulifanya nini katika kupigania wana Kigoma kwa tatizo kama hili kuwaepushia na kuleta afya bora kwa wananchi ...
Inasikitisha kuwa na Vilaza dizaini yako katika Bunge letu tukufu.
Lakini nisikilize Dogo... Sasa Tumepata Jembe ambalo ni la Kiangazi na masika.
Nyie Mafisadi wote mlioifanya nchi ifike hapa Ameshaanza kuwamulika na kuziba mianya yenu yote ya ulaji na msituchafulie Hewa kama mlivyo zoea muaka ile.
Hapa Kazi Tu na si wewe wa kutuambia au wa kutufungia macho.
Zitto cha maana Huna Makonda amefanya aliyo weza akishirikiana na Wazalendo wenzake KWAKO NI KAMA MIUJIZA.
Tula tuli kama maji ya mtungini .... Omboleza watu kukuhama wa Ujuzi wako wa kila kitu ( UTUMBO MTUPU)