Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo amezungumza mambo mengi katika uzinduzi wa programu ya kuifanya Dodoma iwe ya kijani.
Haya ni baadhi ya mambo 9 aliyoyazungumza mjini Dodoma;
-Tupunguze ukataji miti na uvunaji wa miti uzingatie sheria zilizopo.
-Taasisi za serikali zitunge sheria ndogo za kusimamia shughuli za mazingira.
-Wananchi tuitikie na kutekeleza programu mbalimbali zinazoanzishwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
-Hii ni awamu ya kwanza tutaratibu awamu ya pili ya program hii.
-TANROADS iandae utaratibu wa kupanda miti pembezoni mwa barabara.
-Wananchi tuanze kutumia nishati mbadala ili kunusuru mazingira yetu.
-Naagiza kampeni hii isiishie Dodoma Mjini bali ienee katika Wilaya zote za Mkoa huu na hatimaye nchi nzima.
-Upandaji wa miti si kwa ajili ya hifadhi tu bali ni fursa ya kiuchumi pia.
-Kampeni hii ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu Dkt. Magufuli wa kuhamishia Makao Makuu hapa Dodoma.
Alichokisema Makamo wa Rais Katika Uzinduzi wa Kuifanya Dododma Iwe ya Kijani
1
December 21, 2017
Tags
Hivi viongozi nynyi kama viongozi wa kitaifa badala ya kuzungumzia maslahi ya cnhi, Taifa na watu kwa ummoja kwanza. Mnatumia nyazfa zeu kila siku kichama hii inatishia kama mko madarakani kwa kutumia pesa za umma kwa maslahi ya ccm.mnalipwa na Taifa, kodi za kila Mtanzania kukweza kijani, hivi viobgozi wa ccm mnapopewa dhamana na watu wote mnajielewa? Basi gaweni nchi iendeshwe na CCM kwa pesa zenu na si pesa za elimu ya watoto, wanawake wanaozalia chini mahospitali nilitegemea mwanamke kuzungumzia haya kwanza, ni kutekwa tu kutoka ngazi za juu na viongozi wastaafu wote wa ngazi za juu wote mnapigania maslahi ya kijani. Umesahau ZAnzibar mlivyoivuruga, nilifikiri kwa vile ni Mzanzibari utapigania haki za Zanzibar pia. La hasha. Ni kijani , kijani, kijani tu. Tupo tena kwenye uchaguzi ni CCM tu kila kona.upo ccm upo na Magufuli, hupo ccm adui wa Magufuli ndo hivi mnawahubiria watanzania mwisho wa mwaka Christmas. Ni wakati wa kuungana, kutoa ahsantekupanga na kufunga mambo makubwa ya mwaka na wa kesho. Badala yake kijani rangi. Ni aibu gani kutokufikiri makubwa.Tuna watu wenye uchungu na nchi hii au wao ndani ya kijani na maslahi ya kijani tu. Muunge Magufuli, ingia kijani, sauti ya mtu mmoja zidi ya mamilioni ya watu.ingia kijani pata mlo, pata ajira, pata ulinzi, tukutangaze jukwaani na Magufuli kila mtu akuone unavaa kijani. Hizi siasa za kijani vipi. Wapi katiba ya wanchi mama Samia.wapi usawa kwa kila mtu bila kijani. Je hawa wengine si watanzania. Walipa kodi nchini. Je usipokuwa kijani huna mchango sawa. Wengi wasio kijani michango yao ni mikubwa sana kuliko viongozi wengi wa juu wavaa kijani ambao kila siku ni rushwa, mafisadi, madawa ya kulevya wengi wao asilimia themanini mmejificha huko mkivaa kijani.ndo kwenye madhambi mengi ambayo mnashindwa kuyazungumzia badala yake mnashangaa hawa vijana na rusjwa si mmebebana miaka mingi, na sasa wote wameibuka hasa waliokaa kimya kwa muda mwingiwakijua watu wameyasahau madhambi nawaona mnapeana tena vyeo kulinda ngome ya kijani kwa hali na mali. Ni hao hao walituuza.watakuwaje wakweli, mali walioihujumu Tanzania bado wamejilimbikizia na nyingine zinanunua watu majukwaani kweupe.Ndi hii awamu ya tano ya kuua ufisadi ni geresha moja na nyingine.wapo wachache magerezani watatoka tu. Hawa ni wachache sana madingi wao wako majukwaani kuhubiri mchana kwrupe. Ama kweli sis na nchi nzima ni wapumbavu na wajinga watupu.
ReplyDelete