Aunt Ezekiel Awatolea Povu Wanayemsema Kuhusu Kuishi Nyumba za Kupanga

Aunt  Ezekiel Awatolea Povu Wanayemsema Kuhusu Kuishi Nyumba za Kupanga
BAADA ya kuandamwa mitandaoni kuwa tangu amekuwa staa bado anaishi nyumba za kupanga maeneo ya Kijitonyama jijini Dar, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefungukia madai hayo kuwa wengi wanaongea bila kujua undani wa maisha yake.

Akizungumza na Star Mix, Aunt alisema ameamua kuishi maisha ya kupanga kwa sababu ya ukaribu na kazi zake na kama ni nyumba yake ipo maeneo ya Kigamboni.

“Nawashangaa sana wanaosema hivyo. Nimepanga katikati ya mji ili nifanye kazi zangu kwa wepesi na kama ni nyumba mbona ninayo Kigamboni?” Alihoji Aunt ambaye ni mzazi mwenza na Moze Iyobo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad