Haji Manara amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba iondolewe kwa mikwaju ya penati kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) na timu ya Green Warriors, kitendo ambacho kimeonyesha kuwakera na kuwaumiza sana mashabiki wa Simba na wanachama wake ambapo wengi wao walitupa lawama kwa kocha Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon.
