Baada ya Mbunge wa Siha Kuachia Ngazi Chadema Lema Atoboa Siri Wanavyorubuniwa

Baada ya Mbunge wa Siha Kuachia Ngazi Chadema Lema Atoboa Siri Wanavyorubuniwa
Baada ya Mbunge wa jimbo la Siha kupitia tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel leo kutangaza kujivua Ubunge na kuhamia CCM. Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema ametaja marupurupu na vitu ambavyo wabunge kutoka vyama vya upinzani wanavyorubuniwa.

Mhe. Lema ametaja vitu hivyo ikiwa ni masaa machache baada ya Mhe. Mollel kutangaza kujivua nafasi hiyo ya Ubunge.

“Nitakupa mshahara wako wote kwa miaka iliyobaki,pia nitakulipia madeni yako yote,nitakupa kiinua mgongo chako chote nitakupa na mlinzi kwa kipindi hiki na ukitaka tena kugombea nitakupa kipaumbele wewe au kazi nyingine utakayotaka ? Je,utakuwa tayari?Si utakuwa tiyari wajameni?.“ameandika Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Soma na hii – Mbunge wa Chadema ajivua Ubunge, na kuhamia CCM

Awali kulivuma tetesi kuwa Mhe. Lema naye ni moja ya Wabunge wa Vyama vya Upinzani wanaotarajiwa kujiunga na CCM baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuweka picha akiwa na Lema na kuandika maneno yaliyoleta utata.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahahahaha! hayo ni maneno ya mkosaji, wakitoka CCM kwenda chadema ni sawa, ila wakitoka chadema kwenda CCM wamerubuniwa mara wamenunuliwa mara wampewa rushwa!!! Hivi kweli mtu mzima mwenye akili zake timamu na anakipenda chama chake anawezaje kurubuniwa kiasi hicho??? Kwanini ni wao na si'wewe.......NA-BADO...mdogo-mdogo hadi atabaki Mugabe na mkwewe....piiipoozzz PWAAAAAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad