Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.
“Wema alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali. Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi, kwani anatoka wapi?"- Ole Sosopi.
Aliongeza; “Wema hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".
Ole Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu kitakachoiimarisha.
Hata hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba CHADEMA wameweka mipango katika katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe na nauli.
Hahahah! Copy & paste kama kawaida yao.......wapi POLEPOLE
ReplyDeleteMANENO-YA-MKOSAJI, SIZITAKI-MBICHI-HIZI
ReplyDeletekwani amefanya nini toka awe chadema huyo wema? alichosema ni sahihi kabisa atahangaika sana apeleke bangi zake na unga huko huko CCm
ReplyDeletewema alijua uwamuzi aliouchukuwa kuhama ccm ungemsaidia katika matitizo yk kumbe umemuongezea, hahaaa huyu dada ni fungu la kukosa.......na bado aibu anazojitia zinazidi kumdidimiza tu
ReplyDelete