Breaking News: Anna Mgwira Ajitoa ACT Wazalendo Rasmi na Atangaza Kujiunga na CCM

Anna Mngwira Ajitoa ACT Wazalendo Rasmi na Kujiunga na CCM
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Mhe. Anna Mgwira amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha ACT.

Mhe. RC Mgwira aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo kabla ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa na kuachana na nafasi hiyo ndani ya chama hicho na mwanachama wa kawaida.

Mhe. RC Mgwira ametangaza uamuzi huo leo hii wakati wa Mkutano Mkuu wa UWT uliofanyika mjini Dodoma ambapo amesema baada ya kujitakari kwa muda na kufanya kazi na serikali ameona ni muda muhafaka kutamka kuwa anahamia CCM.

“Kwa muda mfupi nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa letu mbele” amesema Mhe. RC Mgwirwa

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Woyoooooooooooo!! KARIBU-KARIBU-MAMA-LA-MAMA, INGIA CCM, PITA UWANI MPAKA CHUMBANI.......CCM OYEEEEEEEEE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad