Breaking News: Mahakama Kuu Yamuachia Huru Sheikh Ponda Katika Kesi ya Kutoa Matamshi ya Uchochezi.

Mahakama Yamuachia Huru Sheikh Ponda Katika Kesi ya Kutoa Matamshi ya Uchochezi.
Mahakama Kuu ya Tanzania imeamuachia huru imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini  Sheikh Issa Ponda dhidi ya rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro kumuachia huru kiongozi huyo.


Sheikh Ponda ameachiwa huru leo mbele ya Jaji Johnson Mkasimongwa ambaye amesema anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.

“Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na mimi nakubaliana na uamuzi huo, hivyo namuachia huru,” amesema Jaji Mkasimongwa

Aidha Jaji Mkasimongwa amefafanua  kwamba upande Jamhri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.

August 10, 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege inadaiwa kwamba Ponda alitoa kauli za kichochezi kwa waumini wa kiislam ambapo mojawapo ya kauli ni ile aliyosema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad