Bushoke Ajipanga Kufanya Ngoma na Papii Kocha

Bushoke Ajipanga Kufanya Ngoma na Papii Kocha
Baada ya muimbaji, Papii Kocha kurudi uraiani na kukutana na rafiki yake Bushoke, wawili hao wanajipanga kuingia studio kwaajili ya kuandaa kazi mpya za muziki.

Bushoke amesema amefurahi sana rafiki yake huyo kuwa huru huku akiahidi kuanza kufanya mchakato wa kumrudisha kwenye game rasmi.

“Nafikiria kufanya naye kolabo,” Bushoke aliliambia Gazeti la Mwanaspoti. “Mungu akijalia ziwe nyingi,  nikifanya shoo napenda ashiriki na vitu vingi napenda nimsaidie ila ziwezi kuviweka wazi,”

Papii Kocha pamoja na baba yake waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad